Dar Kimewaka.
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli, tangu iingie madarakani moja ya ajenda ambayo imekuwa ikisisitizwa ni kuweka mazingira safi ambapo, Rais Magufuli mwenyewe aliongoza kampeni hiyo na kampeni hiyo imeendelezwa na watendaji wengine wa serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. April 30 2016 viongozi mbalimbali, wasanii na wananchi walifanya usafi maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na baadae kufanya matembezi kutoka maeneo ya Ilala, Temeke na Kinondoni na kukutana Leaders Club ambako imezinduliwa rasmi kampeni ya siku 90 ya Dar es salaam kuwa safi. Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda ameizindua kampeni hiyo na amezungumza haya …….. >>>’ tuliacha nafasi ya 2015 na kurudi nyuma kwamba kila mmoja atafanya usafi kwa sababu anajua ni wajibu wake lakini kwa kuwa tumeshindwa kutumia fursa hiyo sasa acha tufanye usafi kwa kushurutishwa na mamlaka tuliyopewa na Rais’ >>>’kamanda Sirr...