Posts

Showing posts from July 6, 2016

NEW VIDEO; Yemi Alade na Sauti Sol wametuletea hii ‘Africa’

Image
  Mtu wangu tuna kila sababu ya kujivunia  muziki wa East Africa kuzidi kuchukua rotation kubwa kwenye Bara la Africa, July 6 2016 Yemi Alade anawashirikisha Sauti Sol kwenye mdundo mpya unaoitwa ‘ Africa ‘ video ikiongozwa na Evie Etseyatse, usisahau pia kuniachia comment yako hapa chini na wakali hawa wataziona hapa

Lionel Messi kahukumiwa miezi 21 jela leo July 6 2016

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi, leo July 6 2016 jina lake limeingia kwenye headlines baada ya hukumu ya kesi yake ya ukwepaji kodi kutoka. Lionel Messi amehukumiwa miezi 21 jela kutokana na kosa la ukwepaji kodi, hukumu hiyo ya Lionel Messi imetoka kutokana na kosa la kutuhumiwa kukwepa kodi pamoja na baba yake mzazi Jorge Messi kati ya mwaka 2007 na 2009, kiasi cha dola milioni 4.5 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 9.8. Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za Hispania kwa watu wanaohukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili, adhabu yao inaweza badilika kutoka kifungo na kulipa faini, hivyo Lionel Messi bado ana nafasi ya kuendelea na maisha yake ya uraiani kama kawaida kama ataamua kulipa faini.

Nyumba ya milioni 700 wanayojenga Navy Kenzo

Image
Biashara ya muziki imekuwa na faida kubwa  ukilinganisha na miaka ya nyuma, nimeipata good news ya wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo ( Aika & Nahreel ) kuhusiana na kuanza ujenzi wa nyumba yao yenye thamani  ya milioni 700, Ayo TV iliwapata Navy Kenzo kuzungumzia nyumba hiyo, pamoja na sehemu ya video ya ujenzi ulipofikia. “Mwaka huu ni mwaka ambao umekuwa wa mafanikio na tumefanya vitu vingi pamoja na tour na tumepata dili nyingi ambazo zimetuingizia pesa, ndio tulikuwa na mipango ya kujenga nyumba toka zamani na imefikia wakati tumeanza kujenga, hii ni nyumba ambayo tumebuni mimi na Aika na itagharimu milioni 700 hadi kuisha”

Cristiano Ronaldo katumia milioni 11 za Tz kununua hii saa.

Image
Cristiano Ronaldo akiwa na kitu kizuri kama viatu ,gari huwa hasiti kukionyesha mtandaoni na hivi karibuni ametuonyesha saa yake aina ya TAG Heuer CARRERA yenye thamani ya dola 5299 za kimarekani ambazo ni kama milioni 11 za pongo. Ronaldo aliandika twitter ‘ Time to relax and bring out my Tag Heuer Carrera to fuel me up before the big match! ‘,  

Harmonize wa WCB kapitia mengi na kwenye hii video kayaimba,’Matatizo’ iko hapa.

Image
  Hii video mpya ya msanii wa WCB Wasafi, Harmonize inaitwa ‘Matatizo’ iko hapa.