Posts

Showing posts with the label Politics

VIDEO: Rais Magufuli alivyojibu Waandishi kwenye Maswali na Majibu IKULU (PART 1)

Image
    November 4 2016 Rais Magufuli alikutana na Waandishi wa habari IKULU , ni baada ya kuwaalika kwenye kutimiza kwake mwaka mmoja toka aingie madarakani na kwenye hii video ( PART 1 ) anajibu maswali waliyomuuliza, tazama hii video hapa chini.

Majibu ya ACT Wazalendo kwa Ole Sendeka baada ya kutaka Zitto achunguzwe

Image
Jana October 28 2016, msemaji wa chama cha mapinduzi ‘CCM’ Christopher Ole Sendeka alikutana na waandshi wa habari pamoja na mambo mengine Christopher Ole Sendeka alimshutumu Zitto Kabwe kwa kile alichosema amekuwa na chuki na serikali ya awamu ya tano, huku akidai alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliokuwa wanasimamia shirika la NSSF wakati akiwa mwenyekiti wa PAC  ambalo hivi karibuni shirika la NSSF limekumbwa na kashfa ya ufisadi hivyo Ole Sendeka ametaka Zitto achunguzwe. Baada ya tuhuma hizo chama cha ACT Wazalendo kimekutana na waandishi wa habari leo October 29 2016 kupitia kwa katibu wa bunge na Serikali za mitaa wa ACT Wazalendo, Habibu Mchange  ambapo amesema wameshtushwa  na tuhuma hizo zilizotolewa na  msemaji wa chama cha Mapinduzi ‘CCM’, Christopher Ole Sendeka dhidi ya Kiongozi wa chama chao,  Zitto Kabwe,  hivyo kutokana na hayo chama cha chao kinakaribisha uchunguzi juu ya mali za Zitto. ’Chama chetu kinakaribisha uchungu...

VIDEO: Siku 330 Rais Magufuli atekeleza hizi ahadi, Zitto aishtukia ripoti ya BOT

Image
kila asubuhi itakua inakuletea uchambuzi wa magazeti ya Tanzania kuhakikisha zote kubwa za siku unazipata, za leo October 2 2016 ziko hapa kwenye hii video.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Vs Freeman Mbowe live

Image
September 8 2016 mkutano wa nne wa bunge la kumi na moja umeendelea tena bungeni Dodoma wakati kazi iliyoanza asubuhi ilikuwa ni maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge kwenda kwa Waziri mkuu Kassim Majaliwa ambapo moja ya wabunge waliopata nafasi ya kuuliza ni pamoja na mbunge wa Hai Freeman Mbowe. Mbowe alitaka kujua sababu za mizingo ya bandarini kukwama na kusababaisha uchumi wa nchi kuanguka…>>>’Kamati ya bunge ilikwenda bandarini, watu wanalalamika uchumi umeanguka sasa serikali mnataka tafiti gani zaidi?‘ –Freeman Mbowe Waziri Mkuu Majaliwa alisimama na kutoa ufafanuzi…>>>’Suala la kushuka kwa usafirishaji wa mizigo kwa njia ya meli imeshuka duniani kote kutokana na kuporomoka kwa bei ya gesi na mafuta, mkakati wetu ni pamoja na kujenga reli ili kusaidia usafirishaji wa mizigo‘ –Waziri mkuu Majaliwa Click to watch.