Posts

Showing posts from September 20, 2016

Maneno makali ya Paul Pogba Kwa mashabiki.

Image
Jumapili ya Septemba 18 2016 klabu ya Man United  ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa tano wa Ligi Kuu England  dhidi ya  Watford  ambao walikuwa wenyeji wa mchezo huo,  Man United  wakiwa ugenini waliruhusu kufungwa magoli 3-1 na huo kuwa mchezo wao wa tatu mfululizo kupoteza. Baada ya kupoteza mchezo huo ambao ulikuwa wa tatu baada ya kupoteza dhidi ya  Man City  katika dimba la  Old Trafford kwa goli 2-1 na kupoteza dhidi ya Feyenoord  katika mchezo wa  Europa League  kwa goli 1-0, presha mitandaoni iliendelea kumuandama  Paul Pogba aliyenunuliwa kwa dau kubwa na kuweka rekodi ya usajili. Kiungo huyo wa  Ufaransa  ambaye hajafanya vizuri bado akiwa na  Man United  toka avunje rekodi ya usajili alitumia account yake rasmi ya instagram kuandika ujumbe kwa mashabiki  “Asante kwa mashabiki wote kuwa pamoja na sisi matokeo bado sio mazuri kwa upande wetu, lakini tunaendelea kupambana, ...