Posts

Showing posts from August 22, 2016

Alikiba alivyoingia kwa surprise kwenye tamasha la Fiesta Mwanza

Image
Ni August 20, 2016  ambapo wakazi wa mkoa wa Mwanza walipata burudani kali kupitia tamasha la Fiesta ambalo liliwakutanisha wasanii wa Bongo Fleva na mkali kutokea Nigeria Wizkid kwenye jukwaa moja viwanja vya CCM Kirumba. Sasa miongoni wasanii waliotoa burudani jukwanii ni hii ya Alikiba alivyoingia kwa suprise huku watu hawakutegemea kama hata ni miongoni mwa watakapanda jukwaani. Itazame hii video hapa  

Tutarajie kazi mpya ya filamu kutoka Mama Kanumba, majibu yako hapa

Image
Kampuni ya usambazaji wa filamu nchini, Steps Entertainment imeipa heshima millardayo.com na Ayo TV kueleza kazi mpya waliyopokea kutoka kwa Bi. Flora Mtegoa (Mama Kanumba) Akizungumza meneja  Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus kayaongea haya>> Ma ma tayari hata juzi tulikuwa nae anasema ana kazi mpya kwahiyo kuna vitu ambazo ameambiwa alete script ili tuhakikishe kazi yake inakuwa nzuri sokoni pamoja na bajeti’ ‘ Hii filamu ina maana itakuwa ya tatu baada ya Kanumba kulikuwa na Malaika kuna filamu nyingine lakini Mama kuna Without daddy hakuwa producer yeye lakini hii itakayokuja atahusika kama mtayarishaji wa filamu kwahiyo kazi ikiwa tayari tutaileta kwenu mashabiki wa filamu’-  Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Meneja Masoko alichokizungumza kuhusu kazi za Mama Kanumba

Maneno ya Nay wa mitego baada ya BASATA kumwachia huru,Je ataendelea kuwachana?

Image
Baada ya Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kumfutia kifungo cha kutojishughulisha na kazi za sanaa msanii wa rap Tanzania,Nay wa Mitego na kumweka chini ya uangalizi maalumu,msanii huyo amedai kuwa ataendelea kuwachana watu kwenye nyimbo zake kama ilivyozoeleka. Akiongea kwenye kipindi cha Funiko Base cha radio 5,Nay amesema kuwa ametumia muda mrefu sana kuwapata mashabiki wake hivyo hawezi kujiwekea mipaka kufanya anachotaka na kudai ataendeleza staili yake ya kuimba ila atafuata maadili zaidi. “ Leo nimemaliza matatizo na BASATA kwa hiyo ni good time kwa mashabiki wangu,kitu ambacho ninawaahidi ni kwamba nitaendelea kuwachana kama kawaida,tutapiga muziki mzuri kama kawaida ijapokuwa hatutavuka mipaka kuwakera watu wengine ” alifunguka Nay ambaye pia amesherekea kumaliza kifungo kwa ngoma mpya inayoitwa good time.

Jose Chameleone amefunguka kwanini hajafanya kolabo na Diamond mpaka leo nakusema

Image
Msanii wa mkongwe wa muziki nchini Uganda Jose Chameleone amefunguka na kusema kuwa hana tatizo lolote linalomfanya asifanye kolabo na msanii wa bongo fleva kutoka Tanzania,Diamond kama watu watu wengi wanavyodhani kuwa wana bifu. Akiongea na mtangazaji wa Kenya, William Tuva wa kipindi cha Mseto,Chameleone amesema kuwa kupishana kwa ratiba yake na Diamond na kila mmoja kuwa busy ndicho kitu hasa kinachofanya kusiwepo na kolabo ya wawili hao “ The problem is,he is busy and I am busy lakini tumwombe Mungu tukipata wakati,it is a very simple thing ”

Maneno ya Diamond Platnumz yanayoashiria ujio wa mtoto wake wa pili

Image
Mkali wa smash hit iitwayo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz amethibitisha ujio wa mtoto wake wa pili kutoka kwa mpenzi wake Zari. Taarifa hizo staa huyo alizitoa leo August 21, 2016 kwenye mtandao wake wa instagram na kuyaandika haya >>> Ukiwa na Mwanamke Mzuri, Superstar, Ambae shilingi Mia miambili haimpigi chenga, Halaf ana akili, Akakuzalia Mtoto wa kike’ ''Halaf mtoto nae Star, halaf akawa na Mimba yako Nyingine ya mtoto wakiume.. basi unajionea Mashia Muruaaaaaaaaaaaaaaaa............. …Lol yani Hapa najikuta kama sjui Biligeti Mzee wa Kwio....... Mi nampenda huyu dada'' - Diamond Platnumz