Posts

Showing posts from July 3, 2016

Pep Guardiola katambulishwa mbele ya mashabiki 5,800 wa Man City,alichosema kuhusu kumsajili Lionel Messi.

Image
Pep Guardiola ’45’ ametambulishwa rasmi kwa mashabiki wa klabu ya Manchester City kama kocha wao mpya. Guardiola mbele ya mashabiki 5,800 kwenye jukwa la shule ya mpira ya Man City Football Academy. Pep Guardiola anaanza mazoezi na Man City Jumatatu ya July 3 2016,Guardiola pia ameongelea tetesi za kumsajili Lionel Messi  kutoka Barcelona nakusema “ Hilo jambo haliko kabisa kwenye mipango yangu “

Ommy Dimpoz na Wayne Rooney kwenye selfie ya pamoja.

Image
Kwenye zile stori za kwenye mitandao ambazo zimefatiliwa sana ni pamoja na hii ya Ommy Dimpoz kukutana na Wayne Rooney mchezaji wa Manchester United wakiwa Ibiza na kisha kupiga picha ambayo imebeba vitu vingi tusivyovifahamu na pengine tulihitaji kufahamu. Picha ambayo imepigwa na Dimpoz ni picha ya video ambayo wanaonekana wanazungumza kitu lakini sauti ya video hiyo imezimwa (mute) so wakati tunasubiri Ommy Dimpoz mwenyewe atuambie walichokuwa wanazungumza ninayo hiyo video mtu wangu ambayo Ommy Dimpoz kapost kwenye akaunti yake ya Instagram. Kwenye post zake Ommy Dimpoz ameonekana akila raha sehemu mbalimbali za Ibiza ,mahali ambako mastaa wengi wa Dunian hutembelea kwa ajili ya mapumziko.