Posts

Showing posts from November 17, 2016

Episode mpya ya Vanessa Mdee ‘Money Diaries’

Image
  Daniel shayo anakuletea kipande hichi cha kipindi cha Vanessa Mdee kinachoitwa "Money Diaries"  Hii ya leo inahusu "Networking" Angalia hapa chini

Biashara nyingine atakayoanzisha Diamond Platnumz hivi karibuni

Image
Manukato itakuwa biashara nyingine atakayokuwa fanya bongo fleva super staa kutoka Tanzania Diamond Platnumz . Kwa sasa amejiunga na mastaa kama Jennifer Lopez na Nicki Minaj ambao tayari wana manukato yao na kila siku wanatengeneza pesa kwa kubuni manukato mengine na kuingiza sokoni kwaajili ya mashabiki zao. Diamond Platnumz anaelekea kuingiza sokoni manukato yake yatakayoitwa # ChibuPerfume #TheScentYouDeserve

VideoMPYA: Chidinma anakualika kuitazama video hii ‘Fallen in Love’

Image
Mwanadada msanii kutokea Nigeria , Chidinma anayefahamika kama ‘Miss Kedike’ ambae ameshafanya collabo na rapper wa Tanzania Joh Makini  kwenye single ya ‘Perfect Combo ‘ amerudi tena kwenye air waves na ngoma yake mpya ya  ‘Fallen in Love’ . Nimekuwekea video ya mdundo huo hapa chini bonyeza play uweze kuitazama …

Rwanda yanunua ndege ya kipekee Afrika nzima, ni ya pili duniani (+Picha)

Image
Huduma za usafiri wa ndege zinazidi kushika kasi kwenye mataifa ya Afrika Mashariki kila siku, Kutoka nchini Rwanda nimeipata hii ya Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir kununua ndege mpya aina ya Boeing 737-800 Next Gen ambayo inatarajiwa kuongeza ushindani wa safari za anga duniani . RwandAir imekuwa kampuni ya kwanza barani Afrika na ya pili duniani kununua ndege ya aina hiyo ambayo imewekwa vifaa vya kuwezesha abiria kutumia huduma za intaneti kwa njia ya Wi-Fi. Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 154 ilitolewa oda ya kununuliwa na Rwanda miaka 6 iliyopita, imetua kwenye uwanja wa ndege wa Kigali November 16, 2016 saa 10 usiku. Waziri wa uchukuzi wa Rwanda Alexis Nzahabwanimana, amesema ndege hiyo mpya itawezesha shirika hilo kupanua safari zake barani Asia, Ulaya na Marekani. Mwezi September mwaka huu, Serikali ya Rwanda ilinunua ndege nyingine ambayo ni ya kwanza Afrika Mashariki aina ya Airbus 330-200, iliyopewa jina la ...