Posts

Showing posts from May 4, 2016

Ted Cruz hataki uraisi

Image
                             Muwania urais wa Marekani Ted Cruz ametangaza kuachana na kampeni za urais kwa tiketi ya chama cha Republican, baada ya kushindwa vibaya na Donald Trump katika kura za Indiana. Bw. Trump ambaye ni mfanyabiashara wa Jijini New York, ambaye si maarufu kwa wengi kwenye chama chake, sasa ni kama amejihakikishia kuteuliwa kuwania urais wa Marekani. Mapema Bw. Cruz alimuiita Bw. Trump kuwa ni mtu muongo ambaye hastahili kuwa rais wa Marekani. Katika mbio za kuwani urais kwa chama cha Democratic, Bw. Bernie Sanders anatarajiwa kumshinda Bi. Hillary Clinton, Indiana.

Video ya Snura - Chura kufungiwa na serikali

May 04 2016 Wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo wamekutana na waandishi wa habari na kutoa tamko la kuufungia wimbo wa Snura ‘chura’ kuchezwa kwenye MEDIA kuanzia leo mpaka hapo Snura atakapoifanyia marekebisho video ya wimbo huo na kutoa wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamii. Sababu za kuufungia ni kinachoonekana ndani ya video ambapo pia Serikali imetangaza kusitisha maonyesho yote ya hadhara ya Snura mpaka atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi zake za sanaa katika baraza la sanaa la taifa BASATA. Akizungumza Kaimu Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini, Zawadi Msalla amesema…….. >>>’ Serikali imesitisha wimbo na video ya chura kupigwa katika vyombo vyote vya habari, maeneo ya wazi na maeneo yote baada ya kuangalia na kuona  miondoko iliyotumika katika utengenezaji wa video ile kwanza ni ya udhalilishaji, aina maadili ya mtanzania na ukiukwaji wa haki za binadamu’.