Posts

Showing posts with the label Social

Rwanda yanunua ndege ya kipekee Afrika nzima, ni ya pili duniani (+Picha)

Image
Huduma za usafiri wa ndege zinazidi kushika kasi kwenye mataifa ya Afrika Mashariki kila siku, Kutoka nchini Rwanda nimeipata hii ya Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir kununua ndege mpya aina ya Boeing 737-800 Next Gen ambayo inatarajiwa kuongeza ushindani wa safari za anga duniani . RwandAir imekuwa kampuni ya kwanza barani Afrika na ya pili duniani kununua ndege ya aina hiyo ambayo imewekwa vifaa vya kuwezesha abiria kutumia huduma za intaneti kwa njia ya Wi-Fi. Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 154 ilitolewa oda ya kununuliwa na Rwanda miaka 6 iliyopita, imetua kwenye uwanja wa ndege wa Kigali November 16, 2016 saa 10 usiku. Waziri wa uchukuzi wa Rwanda Alexis Nzahabwanimana, amesema ndege hiyo mpya itawezesha shirika hilo kupanua safari zake barani Asia, Ulaya na Marekani. Mwezi September mwaka huu, Serikali ya Rwanda ilinunua ndege nyingine ambayo ni ya kwanza Afrika Mashariki aina ya Airbus 330-200, iliyopewa jina la ...

Video ;Mikoa 10 hatarini kupigwa na tetemeko, Saa zahesabika kishindo cha Lugumi

Image
Baada ya matatizo makubwa kuikumba nchi yetu ya Tanzania, mikoa mingine kumi ya tajwa kuwa iko katika hatari ya kukumbwa na tetemeko LA ardhi Angalia video hapo chini

Mkubwa Fella aonyesha nyumba alizowajengea Yamoto band.

Image
Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella ameziweka hadharani nyumba takribani tano za wasanii wake wa kundi la Yamoto Band zilizopo nje ya mji kidogo, Katika kata ya Kisewe. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Fella amesema kuwa ameamua kuziweka wazi  baada ya kusikia maneno mengi kutoka kwa wananchi wakidai kuwa Yamoto Band hawafaidiki na Muziki wanaoufanya. Pia Mkubwa Fella ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa juhudi kubwa sana alizozifanya katika kuhakikisha anafanikiwa kuinua wasanii. Na katika nyumba hizo zitakazozinduliwa hivi karibuni zitapatiwa kwa Wasanii wanne wa Yamoto Band na Mshindi wa BSS 2015 Kayumba Juma.