Posts

Showing posts from May 1, 2016

NAFASI ZA KAZI TANZANIA.. KAMPUNI YA CDL

Image
I. Background: The client is a private, non-denominational, development agency promoting creative solutions to problems that impede social development. The client seeks sustainable solutions to long-term problems of poverty, hunger, literacy and health, with a special emphasis on the needs of rural communities in coastal and other resource-poor areas. The client works in five sectors including Health, Education, Early Childhood Development, Rural Development and Civil Society enhancement. Over the last several years, The client’s programs have evolved and expanded in response to government policies, beneficiary demand and assessment of needs. In order to optimize The client’s efficiency and effectiveness as a development actor in the region, it seeks to support and improve innovations that create viable solutions to community problems that impede development. Are you interested in finding innovative ways to improve education opportunities for children of East Africa? The client ...

Matokeo EPL leo

Image
  Leicester   City wameshindwa kutwaa ubingwa baada ya kushindwa kutamba mbele ya mashetani wekundu Manchester United kwa kutoka safe ya 1-1. Wakati Manchester City imepokea kipigo kilali kutoka kwa Southampton baada ya kupigwa 4-2 Pia Swansea imempiga Liverpool goli 3-1

Wema Sepetu

Image
Madai ya staa mkubwa Bongo aliye pia Miss Tanzania 2006, Wema Isaac Sepetu kwamba wowowo lake linazidi kuwa kubwa kwa sababu anatumia dawa za Kichina yanazidi kushika kasi huku kwa mara ya kwanza mama yake mzazi, Mariam Sepetu akifunguka, Amani limechimba ukweli. MADAI YALIPOANZA Mashoga wanena, alianza na kuongeza unene, sasa kahamia kwenye makalio ili awe na wowowo. Manenomaneno hayo yakazidi kushika kasi zaidi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kitu ambacho kinadaiwa kuikosesha amani familia ya staa huyo na hata yeye mwenyewe. Kulikoni jijini Mwanza, Pati ya Instagram yazua mjadala. Wa mtandaoni wao wanasema Wema anatumia dawa za Kichina kukuza ‘tela’ lake. WEMA ALIPOTAFUTWA Agoma kupokea simu. Agoma kujibu ujumbe. mamawema1Mama Wema MAMA YAKE MZAZI SASA “Nawashangaa wanaomsema vibaya mwanangu kuwa amejaladia (wowowo), wengine wanasema anatumia dawa za Kichani, hakuna ukweli wowote kwani Wema ni mwanangu, namjua alivyo. Hakuna kitu alicho-ongeza kwenye mwili wake.”

Mishahara ya wafanyakazi yapunguziwa kodi

Image
Rais John Magufuli ameshusha kodi ya mapato ya mshahara (paye) kwa wafanyakazi kutoka asilimia 11 mpaka asilimia tisa. Rais Magufuli alitangaza punguzo hilo leo mjini Dodoma alipokuwa akihutubia kwenye siku ya wafanyakazi duniani ambayo kitaifa imefanyika Dodoma. Amesema wafanyakazi wamekuwa waaminifu katika kulipa kodi ambayo inachangia kwenye maendeleo ya taifa kupitia mishahara yao. Alisema kwa kuwa bado vita dhidi ya wafanyakazi hewa na ufisadi inaendelea, ataangalia namna ya kuboresha mishahara yao hapo baadaye. “Niliwaahidi wakati wa kampeni zangu kuwa nitapunguza kodi ya mapato kwenye mishahara yenu; sasa natamka kuwa nashusha kodi kutoka asilimia 11 hadi asilimia tisa. Najua punguzo hilo litakuwa limeacha pengo kwa serikali, lakini tutaangalia vyanzo vingine vya mapato vya kujazia hapo,” alisema Rais Magufuli. Kuhusu wafanyakazi hewa, Rais amesema mpaka jana idadi ya wafanyakazi hewa imefikia 10,295. Amesema wafanyakazi hao hewa wamelipwa zaidi ya Sh 11 bilioni n...

Simba vs Azam

Image
   Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea leo Mei 1 2016 kwa mchezo kati ya Simba dhidi ya Azam FC kuchezwa katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam , huu ni mchezo wa 26 kwa vilabu vyote na ulikuwa mchezo muhimu kwa kila klabu hili kujiweka pazuri katika nafasi ya kuwania ubingwa. Azam FC kabla ya mchezo dhidi ya Simba kumalizika kwa sare ya 0-0 walikuwa na point 58 wakiwa nafasi ya pili ya Ligi, wakati Simba walikuwa nafasi ya tatu wakiwa na point 57 wakiongozwa na Yanga ambao wapo kileleni wakiwa na point 65 na michezo 26. Sare ya mchezo huu ilikuwa ni furaha kwa Yanga ambao wameongeza tofauti ya point kwa Azam FC na Simba . Kwa idadi ya mechi Simba na Azam FC huu ulikuwa ni mchezo muhimu kwao kuhakikisha wanapata point tatu ili kuweza kupunguza tofauti yao ya point na Yanga wanaoongoza Ligi wakiwa na tofauti ya point sita na Azam FC anayefuatia, umuhimu wa mchezo kwa pande zote mbili ndio ulifanya mchezo kuwa na tension kubwa kitu ambacho kilifanya wachezaji wa pande zote ...

SHEESHA SASA BASI.. OFICIALLY FROM THE GOVERNMENT

April 30 2016 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Jenista Mhagama amekutana na waandishi wa habari Dodoma ili kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya dawa za kulevya na namna ya kukabiliana na tatizo hilii. Waziri Mhagama pia amepiga marufuku kwa watumishi wa Hospitali zote kutowauzia dawa za Methadone waathirika wa dawa za kulevya kwakuwa ilishatangaza kuwa ni bure…>>’ Tumetoa onyo kali, na kila mtoa huduma ambaye atakiuka misingi ya huduma hii atachukuliwa hatua ‘ Kama wewe ni mtumiaji wa Shisha hii pia inakuhusu, Waziri Mhagama anasema..>>>’ Tumeanza kufanya utafiti na tumegundua kwamba kuna kila dalili ya matumizi ya dawa za kulevya katika shisha ‘ ‘ Niwaombe Watanzania haswa vijana wanaojihusisha katika matumizi ya shisha katika maeneo ya starehe wachukue tahadhari sana, ni eneo ambalo linapelekea matumizi ya dawa za kulevya ‘

Sakata La Winga Wa Manchester United ya uingereza

Image
Winga mshambuliaji wa klabu ya Man United ya Uingereza Memphis Depay jina lake limeingia kwenye headlines tena, baada ya kufanya kitendo ambacho huenda kikawa na maana ya kuashiria yeye kuondoka au kukosa furaha ndani ya Man United . Memphis amewashangaza wengi hususani mashabiki wake wa Man United wanaomfollow katika account yake ya Instagram, baada ya kuona winga huyo kaamua kufuta picha zote katika Instagram yake zinazohusu Man United ambazo aliwahi kupost na kubakisha moja akiwa na mpenzi wake pekee. Memphis katika account yake ya Instagram amefollow watu 11 pamoja na account ya Man United pekee, kati ya hao hakuna mchezaji mwenzake wa Man United aliyemfollow, kitu ambacho kimeandikwa na mitandao mingi ya Ulaya kuwa huenda winga huyo anataka kuondoka Man United .