Majibu ya ACT Wazalendo kwa Ole Sendeka baada ya kutaka Zitto achunguzwe
Jana October 28 2016, msemaji wa chama cha mapinduzi ‘CCM’ Christopher Ole Sendeka alikutana na waandshi wa habari pamoja na mambo mengine Christopher Ole Sendeka alimshutumu Zitto Kabwe kwa kile alichosema amekuwa na chuki na serikali ya awamu ya tano, huku akidai alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliokuwa wanasimamia shirika la NSSF wakati akiwa mwenyekiti wa PAC ambalo hivi karibuni shirika la NSSF limekumbwa na kashfa ya ufisadi hivyo Ole Sendeka ametaka Zitto achunguzwe. Baada ya tuhuma hizo chama cha ACT Wazalendo kimekutana na waandishi wa habari leo October 29 2016 kupitia kwa katibu wa bunge na Serikali za mitaa wa ACT Wazalendo, Habibu Mchange ambapo amesema wameshtushwa na tuhuma hizo zilizotolewa na msemaji wa chama cha Mapinduzi ‘CCM’, Christopher Ole Sendeka dhidi ya Kiongozi wa chama chao, Zitto Kabwe, hivyo kutokana na hayo chama cha chao kinakaribisha uchunguzi juu ya mali za Zitto. ’Chama chetu kinakaribisha uchungu...