Posts

Showing posts from August 14, 2016

Video: Diamond Platnumz ameshirikishwa na msanii kutoka Zimbabwe kwenye ‘Watora Mari’

Image
Bongofleva inazidi kupata rotation kubwa barani Afrika, Mtu wangu nimekuwekea hii video hapa Diamond Platnumz ameshirikishwa na msanii kutoka  Zimbabwe  ni mdundo uliofanywa na Producer Laizer kutoka WCB wenye jina Watora Mari , usisahau kuniachia comment yako hapa na wakali hawa wataziona hapa. Official Video ya Jah Prayzah ft Diamond Platnumz

Maneno ya Harmonize kwa wanaosema anamcopy Diamond Platnumz

Image
August 11 2016 staa wa muziki wa bongo flava Dully Sykes aliachia video ya mdundo mpya unaoitwa ‘ Inde ‘ ambao ndani yake alimshirikisha staa kutokea laber ya WCB Harmonize ambapo katika baadhi ya comments za mashabiki zilionyesha kumwelekea Harmonize wakidai kuwa kamcopy boss wake Diamond katika style za kucheza pamoja na uvaaji wake. . Sasa leo August 13 2016 Harmonize kupitia account yake ya instagram kaamua kufunguka ya moyoni na kusema…>>>’ Mhhh copy! copy! copy!….. mwisho wa siku hata ukinya utaambiwa kunya kama wewe usimcopy Diamond ebwana mzee  #simbaa video ijayo wacha nianze kuvaa Dera maana nguo zote ushazivaa ‘

ExclusiveVIDEO: Mambo manne atayoyapata Alikiba kwenye mkataba mpya na Sony Music

Image
  Haya mambo manne ni sehemu tu ya mambo ambayo Alikiba atafaidika nayo baada ya kusaini mkataba na kampuni kubwa na maarufu kwenye biashara ya muziki duniani SONY MUSIC , bonyeza play kwenye hii video hapa chini ili kufahamu zaidi

Zlatan Ibrahimovic anavyojitamba kuwa kachangia pesa za usajili wa Pogba Man United

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden ambaye amejiunga na klabu ya Man United msimu huu kama mchezaji huru akitokea klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic , ameingia kwenye headlines baada ya kupost picha ya kiungo Paul Pogba aliyerudi Man United na kuandika maneno ya kuchekesha kidogo. Zlatan amepost picha akiwa na Paul Pogba katika account yake binafsi ya instagram na kuandika “Finally My shirt brought him back @paulpogba” kauli hiyo kwa lugha ya kiswahili ina maana kuwa mauzo yake ya jezi pekee alipojiunga na Man United yametosha kulipa fedha za usajili wa Pogba kutoka Juventus kurejea Man United . Baada ya Zlatan kupost hivyo Pogba nae alimjibu kwa kupost video ya utani instagram wakiwa pamoja na kusema kuwa “this guy wants to get  famous” lakini Zlatan akamjibu kuwa yeye ndio kampost kumfanya apate umaarufu, Pogba ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Bournemouth kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano.