Posts

Showing posts from October 28, 2016

BREAKING NEWS: Usishangae kumuona kocha Hans van Pluijm akiifundisha Yanga tena

Image
  Siku nne baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans muholanzi Hans van Pluijm ajiuzulu nafasi yake hiyo, leo October 28 2016 klabu ya Yanga imemuandikia barua ya kumuomba abadili maamuzi yake ya kujiuzulu na arejee kazini kama kawaida. Baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa kaimu katibu mkuu wake Baraka Deusdedit pamoja na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba ambaye pia ni shabiki wa Yanga na mwanachama, wamemuomba kocha Hans van Pluijm atengue uamuzi wake wa kujiuzulu na kurudi kazini kama kawaida. Kwa maamuzi hayo ya Yanga kumuomba kocha Hans van Pluijm arudi usishangae ukimuona akirejea katika benchi la Yanga kwa siku za karibuni, inaripotiwa kuwa maamuzi ya Yanga kuandika barua hiyo yaliafikiwa baada ya kukaa  na kufanya maongezi na kocha Hans van Pluijm kwa siku tatu pamoja na katibu na waziri Mwigulu   . View image on Twitter

VIDEO ; MATUKIO YA UDANGANYIFU WA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2016

Image
Baraza la mitihani la Taifa limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi ambapo kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2, kabla ya kutangaza matokeo hayo, katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde ameyazungumzia Matukio Sita ya udanganyifu yaliyotokea katika Mtihani wa Darasa la saba 2016. 1. Moja ya matukio ya udanganyifu ni pamoja na la  shule ya msingi Tumaini Sengerema ambapo mmiliki wa shule akishirikiana na wasimamizi alifanya mtihani na kuwapa majibu watahiniwa, wakayaandika kwenye sare zao wakaingia nayo kwenye chumba cha mtihani. 2. Shule ya little flower ambayo iko Serengeti, mwalimu mkuu akishirikiana na wasimamizi waliharibu mtihani wakaufanya na wakawapatia majibu wanafunzi, katika shule hiyo afisa wa baraza alipokuwa akifanya ufuatiliaji wa mitihani alimkamata mwalimu wa shule hiyo ambaye ni msimamizi akiwapa wanafunzi majibu. 3. Shule ya mihamakumi ambayo iko Sikonge mkoani Tabora, walimu walichukua form za kujibia mitihani, wanaf...

VIDEO ; HABARI KAMILI KUHUSU MATOKEO YA DARASA LA SABA 2016

Image
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) jana October limetangaza matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba huku ikionesha kuwa UFAULU umepanda kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka jana hadi asilimia 70.36, huku wavulana waking’ara katika matokeo hayo ambao wengi wametoka shule za Kanda ya Ziwa. Aidha, watahiniwa 238 kutoka shule sita wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika wamefanya udanganyifu katika mtihani huo. Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde alisema kati ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani huo, msichana ni mmoja tu, Justina Gerald wa Shule ya Msingi ya Tusiime ya jijini Dar es Salaam. WANAFUNZI 10 BORA KITAIFA: Ni Japhet Stephano, Jamal Athuman na Enock Bundala (Kwema), Justina na Shabani Mavunde (Tusiime), Jacob Wagine, Isaac Isaac, Daniel Kitundu na Benjamin Benevenuto (Kwema) na Azad Ayatullah (Kaizirege). WASICHANA 10 BORA K...