Posts

Showing posts from September 4, 2016

Mkubwa Fella aonyesha nyumba alizowajengea Yamoto band.

Image
Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella ameziweka hadharani nyumba takribani tano za wasanii wake wa kundi la Yamoto Band zilizopo nje ya mji kidogo, Katika kata ya Kisewe. Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Fella amesema kuwa ameamua kuziweka wazi  baada ya kusikia maneno mengi kutoka kwa wananchi wakidai kuwa Yamoto Band hawafaidiki na Muziki wanaoufanya. Pia Mkubwa Fella ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa juhudi kubwa sana alizozifanya katika kuhakikisha anafanikiwa kuinua wasanii. Na katika nyumba hizo zitakazozinduliwa hivi karibuni zitapatiwa kwa Wasanii wanne wa Yamoto Band na Mshindi wa BSS 2015 Kayumba Juma.

VIDEO; RAYMOND - NATAFUTA KIKI (OFFICIAL VIDEO )

Image
Angalia video mpya ya kijana Raymond a.k.a Rayvany - Natafuta kiki ambae yupo chini ya usimamiza wa WCB under Simba Diamond Platnumz.

Ujumbe mzito wa Chris Brown baada ya tetesi za Lil Wayne kutangaza kuacha muziki.

Image
Baada ya twit kali kutoka kwa Rapa Lil Wayne iliyoashiria kustaafu muziki kwa msanii huyu, rnb staa Chris Brown ametoa ujumbe mzito juu ya mchango wa Lil Wayne kwenye muziki wake. Kupitia Instagram, Chris Brown aliandika hivi “ Lil Wayne amenisaidia sana kwenye muziki wangu, amekuwa mshawishi wangu mkubwa, milele atakuwa rapa mkali zaidi kuwahi kuishi, wasanii wengi wa rapa hata msingejua pakuanzia kama isingekuwa Wayne, wote nyie ni wanafunzi wake hata kama hamtaki kusema, Wayne kaandika nyimbo kibao za wasanii wa Cash Money, mambo yakiwa sawa mnakuwa na sisi ila yaki haribika mnatukimbia “  

Kwa zaidi ya dola laki mbili Chris Brown atoka jela kwa dhamana.

Image
Rnb super staa Chris Brown ametoka jela kwa dhamana ya dola $250,000 usiku wa Jumanne baada ya kukamatwa kwa madai ya kumtishia mwanamke ‘Baylee Curran’ silaha ya moto. Baylee Curran alimshutumu Chris Brown kuwa kamtishia bunduki akiwa nyumbani kwake Tarzana, California. Baylee Curran alikuwa pamoja na mastaa wengine kama Ray J kabla ya ugomvi kuzuka ndani ya nyumba ya Chris. Chris Brown alidaiwa kumfukuza msichana huyo na kumtishia na bunduki kabla hajaondoka. Polisi walifika nyumbani kwa Chris saa tisa alfajiri  baada ya Curran kupeleka mashtaka polisi na kukatolewa hati ya kufanywa msako. TMZ imeripoti kuwa Chris alitupa nje begi dogo lililokuwa na silaha na dawa za kulevya. Chris atapanda kizimbani September 20 mwaka huu.

DIAMOND PLATNUMZ FT NE-YO

Image
Hii ni Video za Diamond Platnumz na Neyo wakiwa kwenye mishe za kukamilisha video ya wimbo wao Marry You . Hii collabo imefanyika Nairobi Kenya wakati Neyo alikuwa kwenye Coke Studio Afrika na Video imefanyika jijini Los Angeles, Marekani.

Video fupi iliyovuja ya Diamond akifanya video na Neyo Marekani

Image
Diamond Platnumz yuko Marekani kwa ajili ya show yake September 2 Los Angeles lakini pia kufanya video ya kolabo na mwimbaji star wa Marekani Neyo ambayo waliirekodi audio yake Nairobi mwaka 2015. BOFYA HAPA KUTIZAMA VIDEO HIYO  

VIDEO: Kwenye Basi la Wasanii Shilole kauliza swali Christian Bella akamtaja Nuh Mziwanda, acha amrukie

Image
Tamasha la FIESTA 2016 lipo kwenye ziara yake ya kutembea kwenye mikoa mbalimbali Tanzania ambapo moja ya vitu ungependa kuona ni jinsi Wasanii wanavyosafiri pamoja kwenye basi na maongezi yao wakati mwingi. Wakati FIESTA ikisubiriwa Jumamosi ya kesho hapa Shinyanga uwanja wa nje wa Kambarage, nakusogezea huu utani kutoka kwenye basi la Wasanii ambapo Shilole kwa utani kuna swali aliuliza kuhusu Wanaume wake alafu Christian Bella akamtaja Nuh Mziwanda ambaye ni mpenzi wa zamani wa Shilole Angalia video kujua kilichoendelea;

VIDEO: Rayvanny alivyowachekesha kina Mr. Blue, Shilole, Chege na wengine kwenye Basi

Image
Tamasha la FIESTA 2016 lipo kwenye ziara yake ya mikoa mbalimbali Tanzania ambapo moja ya vitu ungependa kuona ni jinsi Wasanii wanavyosafiri pamoja kwenye basi na maongezi yao wakati mwingi. Kama hukuwa unajua Rayvanny hana tu kipaji cha kuimba bali hata uchekeshaji vilevile anauweza, kwenye safari wakati wote ameonekana kuwachekesha wasanii wenzake kama inavyoonekana kwenye hii video hapa chini

Staa wa Bongo Movie adaiwa kuzaa mtoto ambaye hajafanana na baba yake

Image
September 02  2016 kwenye U Heard ya Soudy Brown amezungumza na  staa wa Bongo Movie Iren Uwoya kuhusu taarifa zilizosambaa kwenye mitandao kuwa mtoto aliyemzaa si wa mume  wake Ndikumana kwa kuwa hajafanana naye,  millardayo.com imekuwekea full stori.