R.C Paul Makonda na Wafanyakazi Hewa

Mei 2 2016 Mkuu wa mkoa Dar es salaam
Paul Makonda amewaapisha wakuu wa idara na maofisa utumishi wote wa manispaa hiyo ili kusaidia kubaini watumishi hewa.
Makonda kafikia hatua hiyo baada ya watumishi hao kuwa wanampa idadi tofauti kila anapohitaji kupata taarifa, akizungumza na Waandishi wa habari Dar es salaam
Makonda anasema..
>>> ‘Mara ya kwanza mliniambia  tuna watumishi hewa 71, mara ya pili mkasema 87 na mara ya tatu wakapungua hadi 66 tena mara zote hizi ni idadi ya watumishi hewa kimkoa jambo ambalo roho wa Mungu alinikataza kutangaza‘
‘ Sasa Mungu kanipa njia ambayo nimewaambia wiki iliyopita, Leo hii wameongezeka wamefika watumishi hewa 209 huku ziai ya bilioni 2 zikipotea. Je, nisinge msikiliza Mungu si mgenifanya nikafukuzwa kazi? ‘
Baada ya maelezo hayo Mkuu wa mkoa akawapatia mikataba ya viapo katika kutafuta watumishi hewa, lengo likiwa ni kuwataka kila mtumishi kuwabainisha watumishi wao hewa katika idara zao na atakayebainika kutoa taarifa zisizo sahihi mkataba umfunge mwenyewe.

Comments

Popular posts from this blog

NEW VIDEO: Korede Bello - Do like that