Mkubwa Fella aonyesha nyumba alizowajengea Yamoto band.
Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Saidi Fella ameziweka hadharani nyumba takribani tano za wasanii wake wa kundi la Yamoto Band zilizopo nje ya mji kidogo, Katika kata ya Kisewe.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, Fella amesema kuwa ameamua kuziweka wazi baada ya kusikia maneno mengi kutoka kwa wananchi wakidai kuwa Yamoto Band hawafaidiki na Muziki wanaoufanya.
Pia Mkubwa Fella ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa juhudi kubwa sana alizozifanya katika kuhakikisha anafanikiwa kuinua wasanii. Na katika nyumba hizo zitakazozinduliwa hivi karibuni zitapatiwa kwa Wasanii wanne wa Yamoto Band na Mshindi wa BSS 2015 Kayumba Juma.
Comments