Kuhusu milion 50 Za mh. Magufuli
Wakati Rais John Pombe Magufuli akiwania nafasi ya kuiongoza Tanzania aliahidi kutoa shilingi Milioni hamsini kwa kila kijiji .
Leo Mei 10 2016 hoja imeingizwa Bungeni na Mbunge wa viti maalum Esther Mahawe ameuliza Swali…>>’ Je, ni lini fedha hizo zitatolewa? Pili Serikali imejipanga vipi kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wananchi juu ya njia bora ya kutumia fedha hizo? ‘
Nakukutanisha na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Abdallah Possi …>>>’ Serikali imetenga shilingi bilioni 59.5 katika bajeti ya mwaka 2016/2017 chini ya fungu 21 kwa ajili ya kuwezesha wananchi vijijini kwa kutoa shilingi milioni 50 kwa kila kijiji na mtaa‘
‘ Fedha hizo zitatolewa baada ya kuidhinishwa na Bunge na baada ya kukamilisha taratibu zinazolenga kuhakikisha uwepo wa tija katika matumizi ya fedha hizo ‘
‘ Ili kuhakikisha matumizi bora ya fedha hizo Serikali imeendelea kukamilisha maandalizi ya utaratibu maalum wa utoaji fedha hizo ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu ya ujasiriamali‘
Comments