Ted Cruz hataki uraisi


                            Muwania urais wa Marekani Ted Cruz ametangaza kuachana na kampeni za urais kwa tiketi ya chama cha Republican, baada ya kushindwa vibaya na Donald Trump katika kura za Indiana.
Bw. Trump ambaye ni mfanyabiashara wa Jijini New York, ambaye si maarufu kwa wengi kwenye chama chake, sasa ni kama amejihakikishia kuteuliwa kuwania urais wa Marekani.
Mapema Bw. Cruz alimuiita Bw. Trump kuwa ni mtu muongo ambaye hastahili kuwa rais wa Marekani.
Katika mbio za kuwani urais kwa chama cha Democratic, Bw. Bernie Sanders anatarajiwa kumshinda Bi. Hillary Clinton, Indiana.

Comments

Popular posts from this blog

R.C Paul Makonda na Wafanyakazi Hewa

Video: Godzila kafunguka kuhusiana na bifu yake na Billnass