Video ya Snura - Chura kufungiwa na serikali

May 04 2016 Wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo wamekutana na waandishi wa habari na kutoa tamko la kuufungia
wimbo wa Snura ‘chura’ kuchezwa kwenye
MEDIA kuanzia leo mpaka hapo Snura atakapoifanyia marekebisho video ya wimbo huo na kutoa wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamii.
Sababu za kuufungia ni kinachoonekana ndani ya video ambapo pia Serikali imetangaza kusitisha maonyesho yote ya hadhara ya Snura mpaka atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi zake za sanaa katika baraza la sanaa la taifa BASATA.
Akizungumza Kaimu Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini, Zawadi Msalla
amesema……..
>>>’ Serikali imesitisha wimbo na video ya chura kupigwa katika vyombo vyote vya habari, maeneo ya wazi na maeneo yote baada ya kuangalia na kuona  miondoko iliyotumika katika utengenezaji wa video ile kwanza ni ya udhalilishaji, aina maadili ya mtanzania na ukiukwaji wa haki za binadamu’.

Comments

Popular posts from this blog

NEW VIDEO: Korede Bello - Do like that

Diamond Platnumz ameonyesha nyumba yake na Zari Afrika ya Kusini (South Africa )