Portugal / Ureno

Baada ya kusimama kwa takribani siku mbili kwa ajili ya mapumziko ya mechi za Euro 2016, usiku wa June 30 2016 ulichezwa mchezo wa kwanza wa robo fainali ya michuano hiyo ya Euro 2016, mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Euro 2016  ulikuwa kati ya Poland na Ureno.

 Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Stade Velodrome jijini Marseille Ufaransa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya elfu 60, umemalizika kwa timu ya taifa ya Ureno kuibuka na ushindi wa mikawaju ya penati 3-5, hiyo inatokana na dakika 120 kumalizika kwa sare ya goli 1-1, magoli ambayo yalifungwa na Robert Lewandoski dakika ya 2 kwa Poland na Renato Sanchez dakika 33 kwa upande wa Ureno.



 Kwa matokeo hayo Ureno inakuwa timu ya kwanza kufuzu katika hatua ta robo fainali na itakutana na mshindi kati ya Wales dhidi ya Ubelgiji, kama utakuwa unakumbuka vizuri Ureno katika mechi 11 amewahi kuifunga Poland mara 5, sare mara 3 na amewahi kupoteza mara 3 toka October 16 1976. Ureno pia alifuzu hatua ya 16 bora kwa nafasi ya best looser.



https://youtu.be/siK8rlrP8gw
Bonyeza hapa kuangalia video ya penalty.

Comments

Popular posts from this blog

NEW VIDEO: Korede Bello - Do like that