Maneno ya Nay wa mitego baada ya BASATA kumwachia huru,Je ataendelea kuwachana?


Baada ya Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kumfutia kifungo cha kutojishughulisha na kazi za sanaa msanii wa rap Tanzania,Nay wa Mitego na kumweka chini ya uangalizi maalumu,msanii huyo amedai kuwa ataendelea kuwachana watu kwenye nyimbo zake kama ilivyozoeleka.

Akiongea kwenye kipindi cha Funiko Base cha radio 5,Nay amesema kuwa ametumia muda mrefu sana kuwapata mashabiki wake hivyo hawezi kujiwekea mipaka kufanya anachotaka na kudai ataendeleza staili yake ya kuimba ila atafuata maadili zaidi.

Leo nimemaliza matatizo na BASATA kwa hiyo ni good time kwa mashabiki wangu,kitu ambacho ninawaahidi ni kwamba nitaendelea kuwachana kama kawaida,tutapiga muziki mzuri kama kawaida ijapokuwa hatutavuka mipaka kuwakera watu wengine” alifunguka Nay ambaye pia amesherekea kumaliza kifungo kwa ngoma mpya inayoitwa good time.

Comments

Popular posts from this blog

NEW VIDEO: Korede Bello - Do like that