Tutarajie kazi mpya ya filamu kutoka Mama Kanumba, majibu yako hapa
Kampuni ya usambazaji wa filamu nchini,
Steps Entertainment imeipa heshima millardayo.com na Ayo TV kueleza kazi
mpya waliyopokea kutoka kwa Bi. Flora Mtegoa (Mama Kanumba)
Akizungumza meneja Masoko wa Steps Entertainment, Kambarage Ignnatus kayaongea haya>>Mama
tayari hata juzi tulikuwa nae anasema ana kazi mpya kwahiyo kuna vitu
ambazo ameambiwa alete script ili tuhakikishe kazi yake inakuwa nzuri
sokoni pamoja na bajeti’
‘Hii
filamu ina maana itakuwa ya tatu baada ya Kanumba kulikuwa na Malaika
kuna filamu nyingine lakini Mama kuna Without daddy hakuwa producer yeye
lakini hii itakayokuja atahusika kama mtayarishaji wa filamu kwahiyo
kazi ikiwa tayari tutaileta kwenu mashabiki wa filamu’-
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Meneja Masoko alichokizungumza kuhusu kazi za Mama Kanumba
Comments