Kwa zaidi ya dola laki mbili Chris Brown atoka jela kwa dhamana.


Rnb super staa Chris Brown ametoka jela kwa dhamana ya dola $250,000 usiku wa Jumanne baada ya kukamatwa kwa madai ya kumtishia mwanamke ‘Baylee Curran’ silaha ya moto.
Baylee Curran alimshutumu Chris Brown kuwa kamtishia bunduki akiwa nyumbani kwake Tarzana, California. Baylee Curran alikuwa pamoja na mastaa wengine kama Ray J kabla ya ugomvi kuzuka ndani ya nyumba ya Chris.
Chris Brown alidaiwa kumfukuza msichana huyo na kumtishia na bunduki kabla hajaondoka.
Polisi walifika nyumbani kwa Chris saa tisa alfajiri  baada ya Curran kupeleka mashtaka polisi na kukatolewa hati ya kufanywa msako.
TMZ imeripoti kuwa Chris alitupa nje begi dogo lililokuwa na silaha na dawa za kulevya. Chris atapanda kizimbani September 20 mwaka huu.

Comments

Popular posts from this blog

NEW VIDEO: Korede Bello - Do like that