Picha: Ray C kapost muonekano wake mpya instagram
Usiku wa June 16 2016 kuamkia June 17 kuna video ya mwimbaji wa longtime Bongoflevani Rehema Chalamila au Ray C ilisambaa mitandaoni akiwa anachukuliwa na gari la Polisi Kinondoni Dar es salaam ambapo baadae ilikuja kugundulika alipelekwa Hospitali.
Kesho yake mkurugenzi wa vipindi na uzalishajiClouds Media Group Ruge Mutahaba aliongea na Amplifaya ya CloudsFM pamoja namillardayo.com na kuthibitisha kwamba mwimbaji huyu amekubali mwenyewe kwa hiari yake na kupelekwa kwenye nyumba ya matibabu ya kuachana na dawa za kulevya huko Bagamoyo Pwani.
Sasa basi staa huyo akiwa bado yuko Sober House iliyopo Kigamboni leo Sept 7, 2016 amepost muonekana wake mpya kupitia kwenye mtandao wa instagram na kuyaandika haya>Bidii yangu inategemea nguvu yako tu baba’
Comments