VIDEO ; HABARI KAMILI KUHUSU MATOKEO YA DARASA LA SABA 2016
Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi kupitia Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA)
jana October limetangaza matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba huku
ikionesha kuwa UFAULU umepanda kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84
mwaka jana hadi asilimia 70.36, huku wavulana waking’ara katika matokeo
hayo ambao wengi wametoka shule za Kanda ya Ziwa.
Aidha, watahiniwa 238 kutoka shule sita wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika wamefanya udanganyifu katika mtihani huo.
Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji
wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde alisema kati
ya wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri katika mtihani huo, msichana ni
mmoja tu, Justina Gerald wa Shule ya Msingi ya Tusiime ya jijini Dar es
Salaam.
WANAFUNZI 10 BORA KITAIFA: Ni
Japhet Stephano, Jamal Athuman na Enock Bundala (Kwema), Justina na
Shabani Mavunde (Tusiime), Jacob Wagine, Isaac Isaac, Daniel Kitundu na
Benjamin Benevenuto (Kwema) na Azad Ayatullah (Kaizirege).
WASICHANA 10 BORA KITAIFA:
ni Justina na Danielle Onditi (Tusiime), Linda Mtapima (Kaizirege),
Cecilia Kenene (Mugini), Magdalena Deogratias (Rocken Hill), Asnath
Lemanya (Tusiime), Fatuma Singili (Rocken Hill), Ashura Makoba
(Kaizirege), Rachel Ntitu (Fountain of Joy) na Irene Mwijage (Atlas).
WAVULANA 10 BORA KITAIFA:
Ni Japhet Stephano, Jamal Athuman na Enock Bundala (Kwema), Shabani
Mavunde (Tusiime), Jacob Wagine, Isaac Isaac, Daniel Kitundu na Benjamin
Benevenuto (Kwema), Azad Ayatullah (Kaizirege) na Benezeth Hango
(Kwema).
SHULE 10 BORA KITAIFA:
Ni Kwema na Rocken Hill (Shinyanga), Mugini (Mwanza), Fountain of Joy
na Tusiime (Dar es Salaam), Mudio Islamic (Kilimanjaro), Atlas (Dar), St
Achileus (Kagera), Giftskillfull (Dar) na Carmel (Morogoro).
SHULE 10 ZILIZOFANYA VIBAYA:
Ni Mgata, Kitengu, Lumba Chini (Morogoro), Zege na Kikole (Tanga),
Magunga ya Morogoro, Nchinila ya Manyara, Mwabalebi (Simiyu) Ilorienito
(Arusha) na Chohero ya Morogoro.
MIKOA 10 ILIYOONGOZA KITAIFA: Ni Geita, Katavi, Iringa, Dar es Salaam, Kagera, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Njombe na Tabora.
HALMASHAURI 10 BORA KITAIFA: Ni Mpanda Manispaa, Geita Mji, Arusha Mji, Mafinga Mji, Chato, Mwanza Jiji, Moshi Mji, Mji Makambako, Ilemela na Hai.
Comments