VIDEO ; MATUKIO YA UDANGANYIFU WA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2016
Baraza la
mitihani la Taifa limetangaza matokeo ya kumaliza elimu ya msingi ambapo
kumekuwa na ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2, kabla ya kutangaza
matokeo hayo, katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde
ameyazungumzia Matukio Sita ya udanganyifu yaliyotokea katika Mtihani wa
Darasa la saba 2016.
1.
Moja ya matukio ya udanganyifu ni pamoja na la shule ya msingi Tumaini
Sengerema ambapo mmiliki wa shule akishirikiana na wasimamizi alifanya
mtihani na kuwapa majibu watahiniwa, wakayaandika kwenye sare zao
wakaingia nayo kwenye chumba cha mtihani.
2.
Shule ya little flower ambayo iko Serengeti, mwalimu mkuu akishirikiana
na wasimamizi waliharibu mtihani wakaufanya na wakawapatia majibu
wanafunzi, katika shule hiyo afisa wa baraza alipokuwa akifanya
ufuatiliaji wa mitihani alimkamata mwalimu wa shule hiyo ambaye ni
msimamizi akiwapa wanafunzi majibu.
3.
Shule ya mihamakumi ambayo iko Sikonge mkoani Tabora, walimu walichukua
form za kujibia mitihani, wanafunzi wanaingia chumba cha mtihani
kutimiza wajibu tu baadae walimu wanachukua zile karatasi na kuanza
kutoa majibu wao wenyewe
4.Shule
ya Kashi Manyara, mwalimu alijificha chooni akiwa amepanga njama na
mtahiniwa mmoja kwamba atoke na karatasi ya maswali ambapo mwalimu
atafanya na baadaye mwanafunzi arudi chooni kuchukua majibu.
5.
Shule ya St. Getrude Ruvuma, mwalimu mkuu na walimu kadhaa walifanya
njama kuwaonyesha wanafunzi wote ambapo walipanga walimu wakae bwenini
na kwenye nyumba ya mwalimu na wakaweka kikundi cha wanafunzi kadhaa
ambao watakuwa wanapeleka maswali na baadae kuyaendea.
6. Shule kondi pamoja na kasandalala Sikonge watahiniwa walikuwa wote wanakosa kwa namna moja
katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles
Msonde amesema baraza la mitihani Tanzania limeshatoa taarifa ya walimu
na wafanyakazi wengine waliokosa maadili na baraza hilo litafanya
ufuatiliaji wa makusudi kwa wanfunzi waliofaulu hasa watakapochaguliwa
sekondari kuona umahiri wao wa kuwawezesha kufaulu.
Comments