Posts

U HEARD: ‘Mimi ninavyong’anganiwa na wanawake naanzaje kumbaka’-Nay wa Mitego

Image
Stori zilianza wiki iliyopita ambapo Nisha aliandika kuwa ana mimba ya mwanaume ambaye waliachana muda mrefu na baadaye alirudi na kumbaka, hakumtaja jina lake ila akasema ni msanii, kwa mujibu wa taarifa za Soudy Brown mhusika wa mimba hiyo ni Nay wa Mitego. Soudy Brown amepiga stori na Nay wa Mitego…….  '' hizi stori naziona, sipendi kuonekana nashindana na mwanamke, huwa nakaa kimya lakini nimeona vimezidi yeye ana vichochea sijui anatengeneza kiki lakini hii inanichafua, iko hivi mimi sijaonana na huyo msichana karibu mwaka wa tatu sasa, sijui nashirikishwaje kwenye suala la mimba mara naambiwa nimembaka, mimi ninvyogombaniwa na wanawake naanzaje kumbaka'’;- Nay wa Mitego play kusikiliza hapo chini..

FULL LIST: Diamond, Alikiba, Vanessa Mdee, NavyKenzo wametajwa kwenye Tuzo za SoundCityMVP2016

Image
  Mastaa ambao wako A-List kwenye muziki wa BongoFlava kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, NavyKenzo, Vanessa Mde na Alikiba wametajwa kwenye list ya wasanii wanaowania tuzo za SoundCityMVP zinazoandaliwa na kutolewa na kituo cha TV kutoka nchini Nigeria cha Sound City TV. Tayari majina na category zote za wasanii watakawania tuzo hizo yametangazwa na kituo hicho huku zikiwa na ushindani mkubwa kwa namna vipengele vilivopangwa. Diamond Platnumz anawania tuzo mbili ikiwemo Msanii Best African Of The Year pia atachuana na mastaa wengine kwenye tuzo ya “Best Male” ambao ni rapa Emtee kutoka South Africa, Wizkid (Nigeria), Patoranking (Nigeria), Falz (Nigeria), Olamide (Nigeria) na Phyno (Nigeria). Alikiba anawania tuzo ya Video Bora akicompete na mastaa wengine kama Mr. Eazi – SkinTight, Patoranking – No Kissing, Eddy Kenzo – Mbilo Mbilo, Emtee – Roll Up, DJ Maphorisa – Soweto Baby, Phyno – Fada Fada, Olamide – Who You Epp, Harry Song – Raggae Blues na...

Aunty Ezekiel na Mose Iyobo watarajia mtoto wa pili.

Image
Moja kati ya picha ambazo zimekuwa zikisambaa kwa kasi katika mtandao wa Instagram leo Jumamosi ya November 26 ni picha ya muigizaji Aunty Ezekiel pamoja na mpenzi wake Mose Iyobo . Picha hiyo ambayo imepostiwa na baadhi ya watu ikiwemo  Mose Iyobo mwenyewe inamuonesha Aunty Ezikiel akiwa mjamzito, kitu ambacho kimefanya baadhi ya mashabiki wao kutoa comment za pongezi. Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mose Iyobo na Aunty Ezekiel wana mtoto wa kike anayejulikana kwa jina la Cookie hivyo kwa mujibu wa post ya Mose Iyobo inawezekana wakawa wanatarajia mtoto wa pili.

NEW VIDEO: Korede Bello - Do like that

Image
    Good news kwa mashabiki wa staa wa Nigeria chini ya label ya The Mavins , Korede Bello baada ya kuachia collabo yake na Tiwa savage, ‘Mr Romantic ‘ amerudi tena kwenye Air waves na hii ‘Do like that’ ambayo tayari nimekusogezea video yake hapa unaweza kuitazama.

FULL INTERVIEW: Kitu Diamond amesema kuhusu Ommy Dimpoz, nani mkali, Universal, Rihanna na Rick Ross

Image
  Mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz alifanya mahojiano na XXL ya CloudsFM November 23 2016 chini ya Watangazaji B Dozen , Mami Baby na Kennedy na kuongea ishu nyingi kwa uzito ikiwemo kusaini mkataba na Universal, maneno kati yake na Ommy Dimpoz.  

NEW VIDEO: DARASA FT BEN POL - MUZIKI

Image
  Bongofleva inajivunia pia kuwa na Darassa,   wengi wameimba nae sana kwenye hit single ‘ Too Much’ ila leo katuletea hii mpya ya ‘ muziki ‘ kamshirikisha Ben Pol , video imefanywa hapahapa Tanzania na Director Hanscana, ukishaitazama tafadhali usiache kuandika comment yako ili wakipita hapa baadae wajue watu wao wameipokeaje.  

NEW VIDEO ; RICH MAVOKO FT DIAMOND PLATNUMZ - KOKORO OUT NOW!!!

Image
  WCB wanayofuraha kutualika kuitazama video mpya ya kijana wao Rich Mavoko ambayo kamshirikisha Boss wake Diamond Platnumz, ukishamaliza kuitazama video hii ni ruhusa kuacha na comment yako umeionaje na wimbo wenyewe ili wakipita baadae wajue watu wao wameipokeaje.  

NEW VIDEO ; CASSPER NYOVEST FT DIAMOND PLATNUMZ MY HEART

Image
Collabo mpya kutoka kwa Cassper Nyovest na Diamond platmumz wa Tanzania Tazama hapo chini

NEW VIDEO ; DAVIDO FT NASTY C - CCOLEST KID IN AFRICA

Image
Mkali kutoka pande za west Africa "Nigeria" anaejulikana kwa jina la Davido ameachia video yake mpya kabisa .... Itazame hapo chini

VIDEO: Walter Chilambo katangaza kuiacha Bongofleva

Image
  Aliyewahi kuwa mshindi wa Bongo star search mwaka 2012 mkimfahamu kama Walter Chilambo ambae kwa muda kidogo sasa hajatoa ngoma yoyote na hii imejenga maswali mengi kwa mshabiki wake kuwa ameacha muziki ama vipi. Camera za Millardayo.com na AyoTv iliweza kumpata Walter Chilambo na haya ndio maneno aliyozungumza  .. >>> ‘Bongofleva sahizi kiukweli sina plan yoyote kwasababu sahivi plan yangu nataka kuswitch na kufanya kitu kingine haimanishi kwamba naukimbia mziki wa bongofleva hapana! nauweza vizuri sana ila nimekuwa na marafiki wazuri wamenishauri kufanya kitu tofauti hata makanisani pia wachungaji kwahiyo nimekuwa na hofu ya Mungu tu’

VIDEOMPYA: Walter Chilambo ameingia kwenye Gospel, ametuletea ‘Asante’

Image
Baada ya kutangaza kuacha bongofleva Walter Chilambo ameachia video ya wimbo wake mpya wa gospel unaoitwa ‘Asante’. Anatukaribisha kuangalia, pia usiache kuniachia comment yako juu ya wimbo huu ili Walter akisoma ajue watanzania wamepokea vipi wimbo pamoja na video hii.

VIDEO: “Ushindani wa Diamond na Alikiba uendelee”- Bien wa Sauti Sol

Image
Baada ya kundi kutokea nchini Kenya , Sauti Sol kutua Tanzania mkoani Arusha kwaajili ya show itakayofanyika leo Nov 19 2016 Millardayo.com na AyoTv  imeweza kuwapata katika interview na katika maswali waliyoulizwa moja wapo ilikuwa inayosemekana ni beef kati ya Diamond Platnumz na Alikiba. Member wa Crew hiyo Bien Sol amejibu hivi. >>>’Iyo ni biashara na hata sisi Sauti Sol wengine ni mashabiki wa Diamond na wengine wa Alikiba tumefanya nyimbo na Kiba labda wengi hawakufurahi so tutafanya ngoma na Diamond pia iyo bif iendelee cause inacreate job, news, so me naona vyema iyo bif iendelee kwa mtandao tu ni sawa kwasababu kwenye muziki pia kunahitajika ushindani’ – Bien

NEW VIDEO ; TIMBULO FT BARAKA THE PRINCE INAYOITWA "USISAHAU"

Image
Msanii Timbulo leo Nov 18,  2016  ametosogezea hii video ya single mpya iitwayo ‘Usisahau’  aliyomshirikisha Baraka The Prince. Ukishamaliza kuitazama hapa sio mbaya ukituachia na comment yako ili wakali huyo akipita hapa kujua Watanzania wameipokeaje. Tazama hapo chini

U HEARD: Gari ya Mo Music yachukuliwa na Benki kisa deni

Image
U Heard ya XXL leo November 18, 2016 kupitia Clouds FM ipo na stori kuhusu Benki kuchukua gari inayodaiwa ni ya star wa hit single ya Basi Nenda Mo Music. Kwa mujibu wa taarifa ya shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa gari hiyo imechukuliwa na Benki wakati Mo Music akiwa Mwanza. “Sijajua kakamgari ilikuwa yake au ilikuwa ya yule dada aliyekuwa naye kwenye gari, walikuwa kama wanafanya town trip tu ndio jamaa wakatokea wakazuia gari wakashushwa na hao madalali yeye akakimbia ilikuwa ni maeneo ya Cecafa jijini Mwanza. Gari ni aina Verossa. Walikua wanawafatilia kwa nyuma mpaka walivyopaki ndio wakakamatwa.” – Shuhuda  Soudy Brown amezungumza na aliyedaiwa ni baba yake Mo Music na kueleza kile anachokijua yeye kuhusu taarifa hizo. “Hiyo sio kweli kitu ambacho nakizungumza kama sio maneno ya pembeni mimi sina taarifa kwamba Mo amekopa gari sasa kama sina hizo taarifa kwahiyo siwezi kujua kama Moshi (Mo Music ) amenyang’anywa gari hapa mimi niko nyumbani kwangu na ...

Episode mpya ya Vanessa Mdee ‘Money Diaries’

Image
  Daniel shayo anakuletea kipande hichi cha kipindi cha Vanessa Mdee kinachoitwa "Money Diaries"  Hii ya leo inahusu "Networking" Angalia hapa chini

Biashara nyingine atakayoanzisha Diamond Platnumz hivi karibuni

Image
Manukato itakuwa biashara nyingine atakayokuwa fanya bongo fleva super staa kutoka Tanzania Diamond Platnumz . Kwa sasa amejiunga na mastaa kama Jennifer Lopez na Nicki Minaj ambao tayari wana manukato yao na kila siku wanatengeneza pesa kwa kubuni manukato mengine na kuingiza sokoni kwaajili ya mashabiki zao. Diamond Platnumz anaelekea kuingiza sokoni manukato yake yatakayoitwa # ChibuPerfume #TheScentYouDeserve

VideoMPYA: Chidinma anakualika kuitazama video hii ‘Fallen in Love’

Image
Mwanadada msanii kutokea Nigeria , Chidinma anayefahamika kama ‘Miss Kedike’ ambae ameshafanya collabo na rapper wa Tanzania Joh Makini  kwenye single ya ‘Perfect Combo ‘ amerudi tena kwenye air waves na ngoma yake mpya ya  ‘Fallen in Love’ . Nimekuwekea video ya mdundo huo hapa chini bonyeza play uweze kuitazama …

Rwanda yanunua ndege ya kipekee Afrika nzima, ni ya pili duniani (+Picha)

Image
Huduma za usafiri wa ndege zinazidi kushika kasi kwenye mataifa ya Afrika Mashariki kila siku, Kutoka nchini Rwanda nimeipata hii ya Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir kununua ndege mpya aina ya Boeing 737-800 Next Gen ambayo inatarajiwa kuongeza ushindani wa safari za anga duniani . RwandAir imekuwa kampuni ya kwanza barani Afrika na ya pili duniani kununua ndege ya aina hiyo ambayo imewekwa vifaa vya kuwezesha abiria kutumia huduma za intaneti kwa njia ya Wi-Fi. Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 154 ilitolewa oda ya kununuliwa na Rwanda miaka 6 iliyopita, imetua kwenye uwanja wa ndege wa Kigali November 16, 2016 saa 10 usiku. Waziri wa uchukuzi wa Rwanda Alexis Nzahabwanimana, amesema ndege hiyo mpya itawezesha shirika hilo kupanua safari zake barani Asia, Ulaya na Marekani. Mwezi September mwaka huu, Serikali ya Rwanda ilinunua ndege nyingine ambayo ni ya kwanza Afrika Mashariki aina ya Airbus 330-200, iliyopewa jina la ...

U HEARD: Diamond Platnumz atajwa kuhusika kuvunjika uhusiano wa Tunda

Image
U Heard ya XXL ndani ya Clouds FM leo ipo na stori kuhusu kuvunjika kwa uhusiano wa kimapenzi kati ya Video Queen Tunda na mwanaume anayedaiwa kuwa ndiye anayegharamia kila kitu kwenye maisha ya Tunda kuanzia magari, nyumba, simu na starehe zote. Sababu za kuvunjika kwa uhusiano huo imetajwa kuwa ni baada ya Tunda kuanza kutoka kimapenzi na mwimbaji star Diamond Platnumz na weekend iliyopita walikuwa wote Zanzibar kwenye show ya Diamond. Soudy Brown ameipata sauti ya Tunda akijieleza na kujitetea kwa Sponsor wake juu ya kuonekana kwake Zanzibar akiwa karibu na crew ya Diamond Platnumz. “Mimi nilienda Zanzibar sikwenda kwa Diamond nilienda na Posh na bwana ake Posh kama una namba ya Posh mpigie umuulize, Kwani haumjui Posh yule rafiki yangu wa Kariakoo nilikwambia kuna rafiki yangu ana bwana mchina amemuoa. Ndo alinipigia tukaenda wote Zanzibar”;-Tunda

U Heard: Kilichotokea kwenye familia ya Calisah baada ya video yake na Wema Kuvuja

Image
November  14 2016 kwenye U Heard ya Soudy Brown amezungumza na Calisah kuhusu video iliyomuonesha yeye akiwa na  staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu wakikiss, Calisah amesema baada ya video hiyo kuvuja, bibi yake alipoambiwa kwa sababu alikuwa anamtetea sana Calisah alipata mshituko na kufariki…… >>>’Hayo mambo yamesababisha mpaka nimepoteza mtu, amepata presha amefariki leo, siko sawa kabisa imenicost sana hata siwezi kuongea nimepoteza bibi yangu kwa sababu ya hivi vitu imeniumiza sana halafu mimi sijafanya hivyo vitu nivujishe video ili iweje ‘ ;- Calisah